Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 15 Aprili 2016 08:46

HAMAS: OIC ichukue hatua za kuisaidia Palestina

HAMAS: OIC ichukue hatua za kuisaidia Palestina

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imeiomba Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ilisaidie taifa la Palestina katika kukabiliana na uvamizi na ukaliaji wa mabavu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Dk Ahmad Abu Halabiya, mjumbe wa mrengo wa "Mabadiliko na Mageuzi" katika bunge la Palestina wenye mfungamano na harakati ya Hamas, amewataka viongozi washiriki wa kikao cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu kinachofanyika nchini Uturuki watekeleze majukumu na mas-ulia waliyonayo kuhusiana na kuiunga mkono Quds na kuuimarisha muqawama wa Palestina.

Abu Halabiya amesisitizia ulazima wa kufanywa jitihada na kuchukuliwa hatua za kuususia kisiasa na kiuchumi utawala wa Israel na kukomesha harakati zote za kutaka kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo na kuhakikisha viongozi wake wanashtakiwa na kuhukumiwa kwa jinai walizofanya dhidi ya wananchi na ardhi ya Palestina.

Mwanachama huyo mwandamizi wa Hamas amesisitiza pia juu ya umuhimu wa vyombo vya habari vya Kiarabu na vya Kiislamu kuzungumzia zaidi suala la Quds na malengo matukufu ya Palestina.

Katika siku ya kwanza ya kikao cha siku mbili cha viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kilichoanza hapo jana mjini Istanbul, Uturuki, washiriki wa kikao hicho walisisitiza juu ya kuiunga mkono Palestina, kutatuliwa hitilafu baina ya nchi za Kiislamu na kuwa na umoja katika kupambana na ugaidi na misimamo ya kufurutu mpaka.../

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …