Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 05 Aprili 2016 09:04

Washington Post: Maelfu ya Wamerekani wameuawa na polisi ya nchi hiyo.

Washington Post: Maelfu ya Wamerekani wameuawa na polisi ya nchi hiyo.

Gazeti la Washington Post la nchini Marekani limeripoti kuwa polisi ya nchi hiyo imewaua karibu raia 1250 wa nchi hiyo tangu mwaka jana hadi sasa. Kwa mujibu Washington Post, katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka huu wa 2016 polisi ya Marekani imeua raia 256 na mwaka jana iliua raia 990 kwa kuwapiga risasi. Ripoti hiyo imesema kuwa, ukatili wa polisi ya Marekani dhidi ya raia unaongezeka huku jamii ya nchi hiyo ikiendelea kulalamika dhidi ya mwenendo huo wa kikatili wa polisi wanaotumia silaha za moto dhidi ya raia. Maafisa wa polisi ya Marekani wanadai kuwa, idadi kubwa ya raia waliouawa mwaka jana kwa kupigwa risasi na polisi ama walikuwa tishio kwa polisi na raia. Hata hivyo maafisa hao wa polisi ya Marekani wamekataa kuweka wazi majina ya wahanga 210 waliouawa mwaka jana kwa kupigwa risasi na polisi ya nchi hiyo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …