Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 19 Januari 2016 06:44

Wazayuni waendeleza hujuma dhidi ya Palestina

Wazayuni waendeleza hujuma dhidi ya Palestina

Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel jana Jumatatu walimuuwa shahidi kwa kumpiga risasi kijana mmoja wa Kipalestina huko Baitul Laham katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan katika jinai mpya zaidi za utawala huo dhidi ya raia wa Palestina kwa lengo la kukandamiza mapambano ya Intifadha ya Quds.

 

Kwa kuuliwa shahidi kijana huyo Mpalestina, idadi ya mashahidi wa Intifadha ya Quds hadi sasa imefikia 163 tangu kuanza mapambano hayo mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka jana. Maeneo mbalimbali ya ardhi za Palestina tangu mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka jana yamekuwa yakishuhudia maandamano makubwa ya Wapalestina dhidi ya siasa za kichokozi za utawala wa Kizayuni, dhidi ya njama inayoulenga mji wa Baitul Muqaddas na mpango wa kuugawa msikiti wa Al Aqsa. Maelfu ya Wapalestina pia wamejeruhiwa na kutiwa mbaroni katika muda huo wote.
Wazayuni jana Jumatatu waliwatishia kuwauwa na kuwafukuza Wakristo wakazi wa mji wa Baitul Muqaddas. Wakati huo huo Kuhani mmoja Mzayuni ametaka kuungwa mkono suala la kuchomwa moto misikiti na makanisa katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …