Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 30 Julai 2014 10:37

Wapalestina wapenya kishujaa na kumaliza Wazayuni

Wapalestina wapenya kishujaa na kumaliza Wazayuni

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imetoa mkanda wa video unaowaoonyesha wanamamapambano wake wakiwaangamiza wanajeshi kadhaa wa Israel katika shambulizi walilolifanya katika mnara wa doria ya kuchunga moto karibu na eneo la Ukanda wa Ghaza. Mkanda huo wa video uliotolewa jana jioni na harakati ya Hamas unaonyesha picha ya wanajeshi kadhaa wa Israel walioangamizwa na wanamapambano wa Kiislamu hapo juzi.
Makomandoo wa Hamas walitumia njia za chini kwa chini karibu na mpaka wa Ghaza kuushambulia mnara huo wa doria huko Nahal Oz na kufanikiwa kuwaangamiza wanajeshi watano wa Israel. Duru za habari za Israel zimetangaza kuwa hadi sasa wanajeshi 130 wa Israel wamelazwa hospitalini, kumi wakiwa katika hali mahututi. Utawala wa Kizayuni umethibitisha kuangamiswa wanajeshi wake 53 huku harakati ya Hamas ikisema kuwa wanajeshi wa Israel walioangamizwa hadi sasa ni zaidi ya 100. Hamas imeongeza kuwa, hiyo ni idadi ya wanajeshi wa Israel walioweza kuhesabiwa na wanamapambano wake na kwamba idadi ya wanajeshi wa Israel walioangamizwa ni zaidi ya hiyo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …