Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 17 Mei 2014 10:31

Watu 13 wauawa katika shambulizi la kombora Syria

Watu 13 wauawa katika shambulizi la kombora Syria

Watu 13 wameripotiwa kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulizi la kombora lililorushwa na magaidi nchini Syria. Shambulizi hilo lilitokea jana Ijumaa katika eneo la 'al-Ashrafiyyah' mjini Aleppo kaskazini mwa Syria. Aidha jeshi la Syria limeripoti kuwa, limefanikiwa kuyaangamiza makundi ya kigaidi yaliyokuwa na lengo la kupenyeza katika maeneo ya makazi ya raia huko al-Ramusuh mjini Aleppo na katika viunga vingine vya mji huo. Aidha jeshi la Syria limezidi kusonga mbele katika operesheni zake dhidi ya makundi ya kigaidi ndani ya mikoa ya Homs, Daraa na Idlib, ambapo mbali na kuwaangamiza magaidi, pia limefanikiwa kuwatia hasara kubwa magaidi hao. Kwengineko, wagombea wa urais nchini humo wamekosoa muamala wa jamii ya kimataifa kuhusiana na uchaguzi huo. Hassan an-Nuri mmoja wa wagombea urais katika uchaguzi wa nchi hiyo amesema hayo katika mahojiano ya televisheni huku akiashiria harakati za vibaraka wa nje ya nchi zenye lengo la kuzuia kufanyika uchaguzi wa rais wa kidemokrasia nchini humo, amesema kuwa, wagombea urais katika uchaguzi huo wamechaguliwa kwa uhuru. Kwa upande wake, Mahir Hajaar mgombea mwingine katika uchaguzi huo, ameashiria njama za baadhi ya pande za kieneo na kimataifa dhidi ya Syria na kusema, pande hizo zinataka kukwamisha siasa za taifa hilo zinafika  ukingoni na kuiona nchi hiyo inakua sawa na nchi hizo katika demokrasia.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …