Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 22 Machi 2014 12:41

Nigeria kushiriki operesheni ya kurejesha Liberia

Nigeria kushiriki operesheni ya kurejesha Liberia

Serikali ya Nigeria imetangaza kupeleka wanajeshi 700 kwa shabaha ya kushiriki kwenye operesheni ya kurejesha amani na utulivu nchini Liberia. Jenerali Tamunomieibi Dibi mmoja kati ya makamanda wa jeshi la Nigeria amesema kuwa, ushujaa wa majeshi ya Nigeria katika kulinda amani umepelekea kwa jeshi hilo kushiriki kwenye operesheni hiyo ya kurejesha amani Liberia. Jenerali Dibi ameongeza kuwa, hadi sasa Nigeria imeshashiriki kwenye operesheni kadhaa za kuleta amani kama huko Sierra Leone na  katika eneo la Darfur nchini Sudan. Liberia ilikumbwa na machafuko na mapigano ya ndani kuanzia mwaka 1989 hadi  2003. Umoja wa Mataifa umevihifadhi vikosi vyake vya kulinda amani nchini humo kwa tahadhari ya uwezekano wa kuibuka tena mapigano ya ndani nchini humo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …