Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 29 Aprili 2016 20:43

Sayyid Ahmad Khatami: Hatua ya Marekani ya kutwaa dola bilioni 2 za mali ya Iran ni wizi

Sayyid Ahmad Khatami: Hatua ya Marekani ya kutwaa dola bilioni 2 za mali ya Iran ni wizi
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, hatua ya Marekani ya kutwaa dola bilioni mbili mali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ni wizi wa wazi na ni kinyume cha sheria.

Ayatullah Ahmad Khatami ameyasema hayo akijibu uamzi wa mahakama kuu ya Marekani wa kuzuia fedha hizo za Iran na kusisitiza kuwa, viongozi wa Iran kamwe hawatokubali mali ya taifa lao kuporwa, na kwamba, ni jambo lisilo na shaka kuwa, haki ya Iran itarejea nchini kutoka mikononi mwa Marekani. Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran ameashiria pia namna Saudia inavyoendelea kuweka vizuizi kwa raia wa Iran kushiriki katika ibada ya Hija ya mwaka huu na kusema, Makkah na Madina ni miji muhimu ya ulimwengu wa Kiislamu na Aal-Saud hawana haki hata kidogo ya kuwazuia mahujaji wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kufika katika miji hiyo. Amesema kuwa, mahujaji wa Iran hawawezi kushiriki katika ibada hiyo chini ya anga ya kudhalilishwa au bila ya kudhaminiwa usalama wao. Ayatullah Ahmad Khatami aidha amekosoa vikali siasa za Saudia katika eneo la Mashariki ya Kati na kusema kuwa, Aal-Saud ni watekelezaji wa siasa za utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na kwamba, wanaishambulia Yemen kwa lengo la kulinda maslahi ya Israel, kama ambavyo wanatenda jinai nchini Bahrain na kuyaunga mkono makundi ya kigaidi yanayofanya jinai kubwa dhidi ya binaadamu katika nchi za Syria na Iraq.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …