Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 27 Aprili 2016 18:50

Rouhani: Kuzuiwa fedha za Iran huko Marekani ni wizi

Rouhani: Kuzuiwa fedha za Iran huko Marekani ni wizi

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, uamuzi wa Mahakama Kuu ya Marekani wa kuzuia dola bilioni mbili za Iran ni wizi wa wazi na fedheha ya kisheria kwa Marekani na maana yake ni kuendeleza hasama na uadui dhidi ya Iran.

Dakta Hassan Rouhani amesema hayo leo katika kikao na baraza lake la mawaziri na kusisitiza kwamba, serikali ikiwa mwakilishi wa wananchi haitasita hata kidogo kufanya juhudi za kupigania haki za taifa la Iran na kwamba, juhudi hizo zitaendelea mpaka zitakapozaa matunda.

Rais Rouhani amesema kuwa, hii kwamba, mahakama fulani katika kona ya dunia itake kuchukua uamuzi kuhusiana na haki na mali za Iran ni jambo ambalo bila shaka liko kinyume cha sheria na linakinzana na sheria za kimataifa.

Amesema, mashinikizo kama hayo ni fedheria ya kisheria kwa Marekani.

Rais wa Iran amebainisha kwamba, taifa la Iran katu halitafumbia macho haki zake na kuongeza kuwa, kwa miaka mingi maadui wamefanya njama za kulinyima taifa hili haki ya kustafidi na nishati ya nyuklia kinyume kabisa na mikataba ya kimataifa, lakini taifa la Iran limefanikiwa kuchukua haki yake hiyo kutokana na kusimama kwake kidete.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …