Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 27 Aprili 2016 11:49

Wizara ya Kigeni Iran yamwita balozi wa Uswisi Tehran

Wizara ya Kigeni Iran yamwita balozi wa Uswisi Tehran

Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imemwita balozi wa Uswisi mjini Tehran katika kulaani uamuzi wa hivi karibuni wa mahakama kuu ya Marekani dhidi ya nchi hii.

Mohammad Keshavarzadeh, mkuu wa ofisi inayoshughulikia masuala ya Marekani katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, sanjari na kumwita balozi wa Uswisi anayesimamia maslahi ya Marekani nchini Iran, amemkabidhi hati mbili za malalamiko rasmi ya Iran juu ya hatua ya mahakama kuu ya nchi hiyo ya kutumia fedha za Iran kuzilipa fidia familia za askari wa Marekani waliouawa katika shambulizi la miongo kadhaa iliyopita huko Lebanon. Keshavarzadeh ameitaja hatua hiyo kuwa ni ukiukaji wa wazi wa mikataba na makubaliano ya pande mbili ukiwemo mkataba wa 1955 wa nchi mbili na pia mikataba ya sheria za kimataifa ambayo inataka mali za nchi nyingine kulindwa na kuhifadhiwa, ikiwemo mali na fedha za serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Aidha mkuu wa ofisi inayoshughulikia masuala ya Marekani katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, sanjari na kuashiria madai ya mahakama hiyo ya Marekani ya kuituhumu Iran kuwa ilihusika katika mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001 nchini humo, amelaani vikali hatua ya mahakama hiyo ya kuihusisha nchi hii na tuhuma hizo zisizokuwa na msingi. Amesema kuwa tuhuma hizo ni kichekesho hasa kutokana na kwamba, ushahidi uliopo unaonyesha wazi kwamba Iran au raia wake hawakuhusika kwa namna yoyote katika tukio hilo na kusisitiza kwamba madai hayo ni kinyume kabisa na sheria za kimataifa zinazovitaka vyombo vya mahakama kuheshimu haki ya nchi nyingine. Kwa upande wake balozi wa Uswisi anayehusika na maslahi ya Marekani nchini Iran ameahidi kufikisha malalamiko ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na kuifahamisha Iran matokeo yake hapo baadaye.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …