Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 26 Aprili 2016 07:03

Jaberi Ansari: Kuhiji Wairani kutategemea maamuzi ya Saudia

Jaberi Ansari: Kuhiji Wairani kutategemea maamuzi ya Saudia

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hatima ya kushiriki au kutoshiriki Wairani katika ibada ya Hija mwaka huu itategemea maamuzi ya viongozi wa Saudi Arabia.

Shirika la habari la IRNA limemnukuu Sadeq Hossein Jaberi Ansari akisema hayo jana (Jumatatu) mbele ya waandishi wa habari hapa Tehran na kuongeza kuwa, Iran haina tatizo na suala hilo, isipokuwa viongozi wa Saudi Arabia wamekuwa wakikwamisha juhudi hizo.

Amefafanua zaidi kwa kusema, suala hili linategemea maamuzi ya serikali ya Saudia kwani ardhi tukufu za Makkah na Madina zinaendeshwa na serikali hiyo.

Katika maudhui nyingine, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, makubaliano ya kukabidhiwa Tehran mfumo wa kujilinda kwa makombora wa S300 wa Russia yamefikiwa kwa mujibu wa sheria na kwa mujibu wa makubaliano ya nchi mbili na kwamba hivi sasa makubaliano hayo yamefikia daraja ya utekelezaji.

Jaberi Ansari amezungumzia pia suala la kuuzwa maji mazito ya nyuklia ya Iran katika masoko ya kimataifa na kuongeza kuwa, kwa uchache tani 70 za maji hayo zitauzwa katika masoko ya kimataifa na jambo hilo linatambuliwa rasmi na makubaliano ya nyuklia baina ya Iran na kundi la 5+1 maarufu kwa jila na JCPOA.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …