Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 25 Aprili 2016 19:35

Kutoitambua Israel ndio msingi mkuu wa siasa za Iran

Kutoitambua Israel ndio msingi mkuu wa siasa za Iran

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kutoutambua utawala wa Kizayuni wa Israel ni katika misingi thabiti na isiyobadilika ya siasa za mambo ya nje za Jamhuri ya Kiislamu.

Sadeq Hossein Jaberi Ansari amesema hayo leo mbele ya waandishi wa habari hapa mjini Tehran; na amma kuhusiana na baadhi ya nchi za Kiislamu kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni amesema, msimamo thabiti na usioyumba wa Iran tangu mwanzoni mwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kutoutambua wala kuupa uhalali utawala wa Kizayuni na kwamba msimamo huo usiobadilika katika siasa za mambo ya nje za Jamhuri ya Kiislamu bado uko vile vile.

Jaberi Ansari ameongeza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel ni utawala pandikizi na umeundwa ili kulipora taifa la Palestina haki zake. Amesema, utawala huo ndicho chanzo cha migogoro, mauaji, na ugaidi wa kitaasisi katika eneo la Mashariki ya Kati na dunia nzima kwa ujumla.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameongeza kuwa, ana matumaini tawala za nchi za Kiislamu zitazingatia vilivyo mateso wanayoendelea kupata Wapalestina na kuchukua hatua ambazo zitatumikia mustakbali mzuri wa taifa hilo madhlumu.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …