Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 25 Aprili 2016 12:23

Araqchi: Iran itaendelea kupambana ubeberu wa US

Araqchi: Iran itaendelea kupambana ubeberu wa US

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayehusika na masuala ya kisheria na ya kimataifa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya udharura wa kuendelea Iran kupambana na siasa za kibeberu za Marekani.

Sayyid Abbas Araqchi amesema kuwa, utambulisho wa mapatano ya nyuklia ya Iran yajulikanayo kama Mpango wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) hautopelekea kubadilika uhusiano wa Marekani na Iran na kwamba, ukabilianaji wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya siasa za kibeberu na Marekani utaendelea na Wamarekani nao wataendeleza uadui wao.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayehusika na masuala ya kisheria na ya kimataifa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria matatizo yaliyoko katika njia ya kuondolewa haraka vikwazo vya Kibenki na kubainisha kwamba, moja ya sababu za hilo ni ukwamishjaji mambo na kutokuweko uwepesishaji mwafaka wa uhusiano wa Kibenki wa Marekani ambao ulipaswa kuwepo baada ya kufikiwa Mpango wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA).

Abbas Araqchi amesema pia kuwa, moja ya yaliyokuwa malengo ya kiuchumi baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kujiondoa taifa hili na utegemezi wake kwa dola ya Kimarekani na kuasisi uchumi bila dola ya Kimarekani.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …