Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 23 Aprili 2016 20:41

Rouhani: Kutunza mazingira ni jukumu la kiutu, kidini

Rouhani: Kutunza mazingira ni jukumu la kiutu, kidini

Rais Hassan Rouhani amesema mchango wa dini una taathira katika kukuza utamaduni wa kutunza na kuhifadhi mazingira katika jamii za wanadamu.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo leo alipohutubia semina ya pili ya kimataifa ya mazingira, dini na utamaduni iliyofanyika hapa mjini Tehran kwa lengo la kustawisha mazungumzo baina ya tamaduni kwa ajili ya ustawi endelevu. Amesema mazingira yanaweza kuwa wenzo wa kuleta umoja baina ya wafuasi wa dini zote; na ili kuhifadhi mazingira hakuna njia nyengine ghairi ya kuwa na wastani katika mambo na kujiweka mbali na utumiaji mabavu na ubinafsi katika kuamiliana na maumbile.

Rais Rouhani amesisitiza kuwa kuyatunza mazingira ni jukumu muhimu la kiutu, kijamii, kidini na kiutamaduni kwa watu wote na kuongezea kwa kusema: utumiaji wa fueli za kisukuku na vita vya mtawalia vilivyotokea duniani hususan kuanzia karne ya 17 hadi 20 vimesababisha madhara makubwa kwa maumbile.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa ujumbe wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa dunia ni kuwa na kadiri na wastani katika mambo na kila mara inatangaza kwamba njia ya uokovu wa mwanadamu ni kuwa na wastani na kujiweka mbali na ufurutaji mpaka.../

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …