Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 23 Aprili 2016 20:40

Tayyibnia: Iran na Afrika Kusini zitastawisha uhusiano

Tayyibnia: Iran na Afrika Kusini zitastawisha uhusiano

Waziri wa Uchumi na Hazina wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kumeandaliwa mazingira mazuri kwa ajili ya kustawishwa uhusiano kati ya Iran na Afrika Kusini katika nyanja mbalimbali.

Ali Tayyebnia amesema hayo leo hapa mjini Tehran baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Ibrahm Patel Waziri wa Uchumi wa Afrika Kusini na kusisitiza juu ya udharura wa kupanuliwa zaidi ushirikiano wa nchi mbili. Amesema, Iran na Afrika Kusini ni nchi mbili kubwa kabisa na zenye nguvu katika Mashariki ya Kati na kusini mwa Afrika na ambazo zina uwezo mkubwa kwa ajili ya kuwa na mabadilishano na ushirikiano wa kiuchumi.

Waziri wa Uchumi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema pande mbili zimetiliana saini hati ya ushirikiano katika uwanja huo na zimeafikiana juu ya kuweko ushirikiano wa kibenki kati yao.

Wakati huo huo, Bijan Namdar Zanganeh Waziri wa Mafuta wa Iran amesema kuwa, Iran imeanza tena kusafirisha mafuta yake kuelekea nchini Afrika Kusini. Zanganeh amesema hayo katika mazungumzo yake na Tina Joemat-Petterson Waziri wa Nishati wa Afrika Kusini aliyeko safarini hapa nchini.

Waziri wa Mafuta wa Iran amesema pia kuwa, uzalishaji mafuta wa Iran umeongezeka ikilinganishwa na kipindi cha kabla ya kuanza kutekelezwa mapatano ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1 yajulikanayo kama Mpango wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA).

 

 

 

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …