Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 06 Februari 2016 04:48

Canada yaiondolea vikwazo Iran, kufungua ubalozi

Canada yaiondolea vikwazo Iran, kufungua ubalozi

Canada imesema kuwa imeiondolea Iran baadhi ya vikwazo na kwamba inaandaa mazingira ya kuhuisha uhusiano wake wa kidiplomasia na Jamhuri ya Kiislamu.

Serikali ya Justin Trudeau, Waziri Mkuu wa Canada imeyasema hayo jana Ijumaa na kuongeza kuwa, imeangalia upya uhusiano wake na nchi hii na kwamba sasa itayaruhusu tena makampuni ya nchi hiyo kuja hapa nchini kuwekeza. Taarifa ya serikali ya Canada iliyosomwa na Stephane Dion, Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo imesisitiza kuwa, itachukua hatua za haraka kuhuisha uhusiano wa kidiplomasia na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Mwishoni mwa mwezi uliopita wa Januari, Dion aliliambia bunge la nchi hiyo kwamba serikali inaharakisha mchakato wa kuondoa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada pia amesema ubalozi wa nchi hiyo utafunguliwa tena hapa mjini Tehran na hivyo kuhuisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya pande mbili.

Tangu kuondolewa rasmi vikwazo vya kidhulma dhidi ya Iran, nchi nyingi za Magharibi zimetangaza utayarifu wao wa kuwekeza hapa nchini na kuhuisha uhusiano wa kiuchumi na kisiasa na Tehran.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …