Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 14 Oktoba 2015 19:22

Kambi za makombora zilizoko mita 500 chini ya ardhi

Kambi za makombora zilizoko mita 500 chini ya ardhi

Kamanda wa kikosi cha anga za juu cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kambi za makombora za jeshi hilo zilizoko umbali wa mita 500 chini ya ardhi ziko tayari wakati wote kwa ajili ya kukabiliana na vitisho vya maadui.
Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh, amesema hayo leo wakati alipohojiwa na shirika la habari la IRIB na kuongeza kuwa, makombora ya masafa tofauti ya jeshi hilo yako tayari katika kambi zote kwa ajili ya kufyatuliwa, na yanasubiri amri tu ya Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Brigedia Jenerali Hajizadeh amesisitiza kuwa, Iran haina wasiwasi wowote katika kukabiliana na satalaiti na zana za kisasa kabisa za kijasusi na mashambulizi za maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusisitiza kuwa, hakuna kitisho chochote kitakachoweza kutishia usalama wa Iran, kutoka nje ya nchi hii.
Kamanda wa kikosi cha anga za juu cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Sepah ameongeza kuwa, licha ya kwamba Iran imezungukwa na nchi zenye machafuko, lakini ina utulivu kamili na kusisitiza kwamba, hayo ni matunda ya juhudi za usiku na mchana za vikosi vyote vya ulinzi vya Iran, vya Sepah, Basiji, Jeshi na Polisi na amewahikishia wananchi wa Iran kuwa adui hathubutu kulifanya chochote taifa lao.
Kamanda Hajizadeh amesisitiza kuwa, Iran si nchi ambayo inaweza kuanzisha vita dhidi ya nchi nyingine, lakini kama itatokezea nchi na kufanya kosa la kuishambulia Jamhuri ya Kiislamu, basi makombora ya Iran yaliyoko chini kabisa ya ardhi yatafyatuliwa haraka na kuwa mithili ya volkano, na hilo litakuwa ni balaa kubwa kwa adui.

Ingia hapa chini kuangalia video kuhusu habari hiyo

 

Picha zinapatikana pia hapa

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Sauti na Video

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …