Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 19 Aprili 2015 20:43

Rouhani: Tutastawisha ushirikiano na Afghanistan

Rouhani: Tutastawisha ushirikiano na Afghanistan

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa biashara kati ya Iran na Afghanistan ni miongoni mwa mipango mikuu ya kustawisha uhusiano kati ya nchi mbili. Rais Hassan Rouhani amesisitiza hayo leo hapa Tehran kwenye kikao cha pamoja cha ujumbe za ngazi za juu wa Iran na Afghanistan na kusisitiza kuwa: Kadiri Afghanistan itakavyokuwa na usalama na amani zaidi na kustawi zaidi, ndipo mabadilishano ya kiuchumi na hatimaye maingiliano mazuri zaidi ya kijamii yataongezeka, jambo ambalo litakuwa ni kwa maslahi ya nchi mbili.
Katika kikao hicho, Rais Rouhani amepongeza utendaji wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Afghanistan katika kurejesha amani na kuyashirikisha makundi na makabila yote ya nchi hiyo na kuongeza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran siku zote imekuwa pamoja na wananchi wa Afghanistan kwa shida na raha. Rais Hassan Rouhani ameashiria mazungumzo ya Iran na Afghanistan kuhusu haki za maji ya mito iliyoko mipakani na kuongeza kuwa nchi mbili zinapaswa kuandaa fremu maalumu kuhusu kadhia hiyo ili haki na uadilifu utendeke.
Kwa upande wake Rais Muhammad Ashraf Ghani wa Afghanishatn amesema: Iran na Afghanistan zina mipaka yenye amani na ametaka kustawishwa ushirikiano wa nchi mbili katika nyanja za pande mbili, kieneo na kimataifa. Rais wa Afghanistan amesema kuwa nchi yake haitaruhusu kutumiwa ardhi ya nchi hiyo dhidi ya nchi jirani na kuongeza kuwa serikali ya Afghanistan imedhamiria vilivyo kustafidi na fursa zilizopo ili kuimarisha amani, ushirikiano, huduma za kijamii na utulivu kwa ajili ya wananchi wa Iran na Afghanistan.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …