Jumatatu, 20 Mei 2013 21:23

Tsvangirai: Nikishinda urais uwekezaji utaimarika

Tsvangirai: Nikishinda urais uwekezaji utaimarika

Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai amesema kuwa iwapo atashinda uchaguzi mkuu ujao wa rais atafuta sheria iliyopitishwa mwaka 2010 inayowalazimisha wawekezaji wa kigeni kuuza zaidi ya asilimia 50 ya hisa zao kwa raia wa Wazimbabwe. Tsvangirai amesema sheria hiyo ilipitishwa kwa jazba na matokeo yake hadi sasa yamekuwa na athari mbaya kwa uchumi wa nchi. Morgan Tsvangirai ambaye ametangaza nia yake ya kuwania urais amesema Zimbabwe inawahitaji wawekezaji wa kigeni ili uchumi uimarike. Hata hivyo amesisitiza kuwa, Wazimbabwe pia watapata nafasi ya kuwa na hisa katika makampuni ya wageni. Uchaguzi wa rais nchini Zimbabwe unatarajiwa kufanyika badaye mwaka huu.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Uvimbe katika mfuko wa uzazi (Fibroid)

Assalam Aleykum wasikilizaji wapenzi na karibu kujiunga nami katika kipindi kingine cha Ijue Afya Yako. Leo tutaendelea kujadili magonjwa yanayowasumbua …

Utawala wa Kizayuni, Mzaliwa wa Ugaidi (6)

Ni matumaini yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji popote pale mlipo. Karibu katika sehemu nyingine ya makala hii ya Utawala wa …

Uislamu na Mtindo wa Maisha (37)

Karibuni kuwa nasi tena katika sehemu nyingine ya kipindi cha Uislamu na Mtindo wa maisha. Kipindi chetu cha leo kitazungumzia …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (4) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …