Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 10 Aprili 2016 08:44

84 waaga dunia katika mkasa wa moto nchini India

84 waaga dunia katika mkasa wa moto nchini India

Kwa akali watu 84 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa katika mkasa wa moto uliotokea mapema leo katika mji bandari wa Kollam, kusini mwa India.

Habari zinasema kuwa, moto huo uliotokea katika Hekalu la Puttingal katika kitongoji cha Paravur jimbo la Kerala, ulisababishwa na kuripuliwa mafataki, wakati wa maandalizi ya sherehe za Vishu, za kuadhimisha mwaka mpya wa jamii ya Wahindu. Sherehe hizo zinazojulikana kama ‘Hafla za Mwanga na Fataki’ zinatazamiwa kufanyika Aprili 14.

Waziri wa Masuala ya Ndani wa jimbo la Kerala, Ramesh Chennitah amethibitisha kutokea mkasa huo na ameagiza maafisa usalama kushirikiana na timu za waokoaji ili kuokoa manusuru na kuwapeleka hospitalini.

Vyombo vya habari vya India vimeripoti kuwa, kwa sasa moto huo umedhibitiwa na manusura wamekimbizwa katika hospitali ya mji wa Thiruvananthapuram, makao makuu ya jimbo hilo.

Itakumbukwa kuwa, tarehe Mosi Januari mwaka huu, watu kadhaa waliaga dunia katika mkasa mwingine wa moto wa kukaribisha mwaka mpya mjini Dubai, katika Umoja wa Falme za Kiarabu. Moto huo ulizuka baada ya kuripuliwa mafataki ya kuukaribisha mwaka mpya kwenye Hoteli ya Adress Downtown yenye ghorofa 63 na iliyoko karibu na jengo refu zaidi duniani la Burj al-Khalifa.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …