Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 02 Machi 2016 10:45

Waislamu India wapinga uchochezi wa Wahindu

Waislamu India wapinga uchochezi wa Wahindu

Waislamu wa India wamefanya maandamano mjini New Delhi wakipinga vitendo vya kichochezi vinavyofanywa na Wahindu wenye misimamo mikali.

Waandamanaji hao wametoa wito wa kukabiliana ipasavyo na Wahindu hao wenye misimamo mikali ili kuzuia machafuko na ghasia baina ya wafuasi wa dini na madhehebu mbalimbali nchini India.

Shabnam Hashimi ambaye ni miongoni mwa viongozi wa maandamano hayo amelaani matamshi ya kichochezi yaliyotolewa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Rasilimali Watu wa serikali ya India dhidi ya Waislamu na ametoa wito wa kutimuliwa kazi waziri huyo.

Siku chache zilizopita Waziri wa Maendeleo ya Rasilimali Watu wa India, Ram Shankar Katheria alihutubia mkutano katika mji wa Agra katika jimbo la Uttar Pradesh akitangaza vita dhidi ya Waislamu. Waziri Ram Shankar alitoa matamshi hayo baada ya watu wasiojulikana kuua kiongozi mmoja wa kieneo.

Matamshi hayo yasiyo ya kuwajibika yamelaaniwa na vyama mbalimbali vya siasa nchini India.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …