Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 26 Januari 2016 06:34

Marekani, Israel ni waratibu wakuu magaidi matakfiri

Marekani, Israel ni waratibu wakuu magaidi matakfiri
Mkuu wa Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: "Marekani na Israel ndilo chimbuko la makundi la kigaidi na kitakfiri."

Hujjatul Islam Walmuslimin Mohammad Mohammadi Golpaygani, amebainisha hayo na kuongeza kuwa: "Makundi ya wakufurishaji kama vile Daesh (ISIS), Jabhat Nusra, Taliban na al Qaeda yameundwa na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel ili waweze kufikia malengo yao katika eneo hili."

Akizungumza Jumatatu, Mkuu wa Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: "Mabeberu na Uzayuni wa Kimataifa wanalenga kuvuruga itikadi za vijana wa Iran ili kuondoa moyo wa kufa shahidi na ujasiri wao."

Hujjatul Islam Walmuslimin Golpaygani ameashiria barua mbili za hivi karibuni za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi kwa vijana wa Magharibi na kusema kuwa: "Vijana wana fikra na dhamiri safi na wana azma ya kutafuta ukweli. Hii ni katika hali ambayo wanasiasa wakongwe wa nchi za Magharibi wanaficha ukweli ili usiwafikie vijana." Aidha amesema vijana wa nchi za Magharibi wanapaswa kufahamishwa ukweli kuhusu njama za watawala wa nchi zao kuhusu chuki dhidi ya Uislamu."

Hujjatul Islam wal Muslimin Golpaygani amesema: "Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu anawahimiza vijana Wamagharibi wausome Uislamu kutoka vyanzo vyake asili na pia waisome Qur'ani Tukufu kwani inasisitizia kuheshimiwa ubinadamu."

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …