Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 05 Januari 2016 06:51

Mamia waandamana Indonesia kulaani Aal Saudi

Mamia waandamana Indonesia kulaani Aal Saudi

Mamia ya watu wamefanya maandamano mbele ya ubalozi wa Saudia nchini Indonesia, katika kulaani kitendo cha kuuawa shahidi Sheikh Nimr Baqir al-Nimr kilichofanywa na watawala wa Aal Saud

Maandamano hayo yaliyofanyika jana (Jumatatu) huko Jakarta, mji mkuu wa Indonesia yamehudhuriwa na wanaharakati wa haki za binaadamu na wanafunzi wa vyuo vikuu, ambapo walipaza sauti katika kulaani vikali hatua ya utawala wa Aal Saud kumnyonga mwanachuoni wa Kiislamu Sheikh Nimr Baqir al-Nimr. Waandamanaji hao waliokuwa wamebeba maberamu na mabango yaliyokuwa na jumbe mbalimbali katika kulaani utawala wa Riyadh, wamezitaka taasisi za kimataifa kukomesha haraka iwezekanavyo miamala ya kuchupa mipaka ya Saudia. Aidha Waindonesia hao waliokuwa wamebebelea picha za shahid Sheikh Nimr, wameitaja hatua hiyo ya watawala wa kifalme wa Saudia kuwa ni alama ya kushindwa kukabiliana na upinzani wa amani. Waandamanaji wamesisitiza kuwa, nchi zinazojinadi kuwa watetezi wa haki za binaadamu, zinatakiwa kuchukua hatua za kivitendo ili kuhitimisha ukandamizaji uliokithiri nchini Saudi Arabia. Wamesema kuwa, Riyadh inafuata kikamilifu siasa za utawala wa Kizayuni wa Israel na kusisitiza kuwa, mauaji ya Sheikh Nimr yamebainisha wazi namna watawala wa Riyadh walivyo mbali na maslahi ya Kiislamu.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …