Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 15 Disemba 2015 11:28

Kashmir yapongeza barua ya Kiongozi Muadhamu

Kashmir yapongeza barua ya Kiongozi Muadhamu

Baruaya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei kwa vijana wa Magharibi imeendelea kumimiwa sifa na kupongezwa kote duniani. Wananchi wa eneo la Kashmir ambalo liko chini ya udhibiti wa India, wameipongeza barua hiyo na kusema kuwa imekuja wakati mwafaka, kipindi ambacho ulimwengu unapokea habari za kupotosha na za kipropaganda kuhusu Uislamu.

Mwandishi wa kanali ya televisheni ya Press TV ya Iran, Syed Ali Safvi amesema wananchi wa Kashmiri wameipongeza barua hiyo ya Kiongozi Muadhamu na kusema kuwa itachangia pakubwa kuufahamisha ulimwengu kuhusu misimamo ya undumakuwili ya nchi za Magharibi katika suala la ugaidi. Ikumbukwe kuwa Ayatullah Khamenei Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu tarehe 29 mwezi uliopita wa Novemba aliandika barua kwa vijana wa Magharibi na akasema aliandika barua hiyo kufuatia matukio machungu ya kigaidi hasa ya Ufaransa tarehe 13 mwezi uliopita. Barua hiyo ambayo ni ya pili kwa vijana wa Magharibi baada ya ile ya Januari imeendelea kuakisiwa kote duniani huku wasomi na vijana wanaharakati wakisema imekuja wakati unaofaa kwani kunaenea chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi pasina vijana wa nchi hizo kujua ukweli kuhusu Uislamu na Waislamu.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …