Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 23 Novemba 2015 11:50

Daesh yatishia kufanya mashambulizi Bangladesh

Daesh yatishia kufanya mashambulizi Bangladesh

Kundi la kigaidi la Daesh limetishia kufanya mashambulizi nchini Bangladesh.
Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh limetangaza kwenye gazeti lake la Dabiq kuwa linaionya serikali ya Bangladesh kuwa itaendeleza mashambulizi yake kama njia ya kuongeza nguvu zake nchini humo.
Vile vile kundi la kigaidi la Daesh limedai kuwa, serikali ya Bangladesh inachuja habari na kuficha ukweli wa mambo.
Siku ya Ijumaa, kundi la kitakfiri la Daesh lilitangaza kuhusika na ufyatuaji risasi dhidi ya daktari na kasisi mmoja kutoka Italia na kudai kuwa hilo ni shambulizi la tatu kufanywa na genge hilo dhidi ya wageni nchini Bangladesh
Hata hivyo serikali ya Bangladesh imekanusha madai hayo ikisema kuwa, wapinzani ndio waliofanya mashambulizi hayo ili kuishinikiza serikali.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …