Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 11 Novemba 2015 08:36

Maandamano Afghanistan kulaani mauaji ya Mashia

Maandamano Afghanistan kulaani mauaji ya Mashia

Maelfu ya wananchi wa Afghanistan wamefanya maandamano kupinga wimbi la mauaji ya kiholela dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia, linaloendelezwa na kundi la kitakfiri la Daesh.

Waandamanaji hao waliomiminika katika barabara za mji wa Ghazni, wamelaani vikali hatua ya Daesh kuuwa Waislamu saba wa Kishia wa jamii ya Hazara katika mkoa wa kusini wa Zabul. Aidha maandamano mengine ya kukosoa ukatili huo yamefanyika katika mji wa Kabul.

Haya yanajiri siku chache baada ya Rais Ashraf Ghani wa nchi hiyo kulaani vikali mauaji hayo. Rais Ghani alisema amehuzunishwa sana na mauaji hayo na kusisitiza kuwa mauaji ya kikatili dhidi ya raia wasio na hatia hususan wanawake na watoto hayawezi kuhalalishwa katika dini au imani yoyote ile. Vilevile ameapa kuwa atahakikisha waliohusika na jinai hiyo wanapatikana na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

 

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …