Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 06 Novemba 2015 08:46

MSF: Marekani ilikusudia kuua watu Kunduz

MSF: Marekani ilikusudia kuua watu Kunduz

Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) imetangaza kuwa shambulizi lililofanywa na ndege za kivita za Marekani dhidi ya hospitali ya jumuiya hiyo katika mji wa Kunduz nchini Afghanistan lilifanyika kwa makusudi kwa ajili ya kuua watu na kufanya uharibifu.
Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Christopher Stokes ambaye alikuwa akitoa ripoti ya uchunguzi kuhusu shambulizi hilo amesema lilifanyika kwa makusudi ya kuua watu na kufanya uharibifu. Ripoti ya shirika hilo imeeleza jinsi wagonjwa na wahudumu wa hospitali hiyo ya Kunduz walivyoungua kwa moto na kuteketea kutokana na shambulizi hilo la Marekani. Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka linasema kuwa shambulizi hilo la Marekani dhidi ya hospitali ambalo limeua raia wasiopungua 30, ni jinai ya kivita na limetoa wito wa kufanyika uchunguzi huru kuhusu maafa hayo. Taarifa hiyo imetolewa baada ya Rais Barack Obama wa Marekani kuomba radhi kuhusu jinai hiyo na kudai kuwa ilifanyika kimakosa. Shambulizi hilo la Marekani lililolenga hospitali nchini Afghanistan limelaaniwa vikali na jumuiya nyingi za kimataifa na nchi mbalimbali duniani.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …