Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 06 Novemba 2015 08:44

Wasaudia waandamana kumtetea Sheikh Nimr

Wasaudia waandamana kumtetea Sheikh Nimr

Wananchi wa maeneo ya mashariki mwa Saudi Arabia wamefanya maandamano wakimuunga mkono mwanazuoni wa Kishia anayehukumiwa kifo na mahakama za Saudia Arabia, Sheikh Nimr Baqir al Nimr baada ya kukosoa vikali sera za kibaguzi za serikali ya Riyadh.
Wananchi wa mji wa Awwamiyyah walifanya maandamano jana usiku wakipinga hukumu hiyo ya kifo na kutaka mwanazuoni huyo wa Kiislamu na wafungwa wengine wa kisiasa nchini Saudia waachiwe huru.
Waandamanaji hao ambao walikuwa wakipiga nara dhidi ya serikali ya Riyadh wametoa wito wa kufutwa hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya msomi huyo anayetetea uhuru na haki za binadamu na maelfu ya wafungwa wa kisiasa wanaoshikiliwa katika korokoro za Saudi Arabia.
Mahakama Kuu ya Saudi Arabia imepasisha hukumu ya kifo iliyotolewa na mahakama moja ya nchi hiyo dhidi ya msomi huyo na utekelezaji wake unasubiri saini ya Mfalme Salman bin Abdulaziz. Sheikh Nimr Baqir al Nimr ambaye amekuwa akipigania haki za binadamu hususan Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaokandamizwa sana nchini Saudia alikamatwa mwaka 2011 katika mji wa mashariki mwa nchi hiyo wa Qatif.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …