Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 04 Novemba 2015 14:12

MSF: Shambulizi la US dhidi ya hospitali ni jinai ya vita

MSF: Shambulizi la US dhidi ya hospitali ni jinai ya vita

Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka MSF, kwa mara nyingine tena limekosoa shambulizi la anga lililofanywa na jeshi la Marekani dhidi ya hospitali moja nchini Afghanistan.
Akizungumza mjini New York nchini Marekani wakati wa maandamano ya kuadhimisha mwezi mmoja tokea lifanyike shambulizi hilo, Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo liliso la serikali amesema shambulizi hilo linapaswa kuendelea kulaaniwa na jamii ya kimataifa na kwamba lilichupa mipaka ya vita, akisisitiza kuwa 'vita pia vina kanuni.'
Waandamanaji hao waliokuwa na ghadhabu hapo jana walitoa wito wa kufanyika uchunguzi huru na wahusika kuwajibishwa kisheria mara moja. Mapema mwezi uliopita, Rais Barack Obama wa Marekani alilazimika kuomba radhi kufuatia shambulizi hilo lililofanywa na jeshi la nchi hiyo dhidi ya hopistali moja katika mji wa Kunduz nchini Afghanistan. Raia 30 wakiwemo wafanyakazi 12 wa shirika hilo waliuawa katika shambulizi hilo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …