Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 02 Novemba 2015 09:09

Waandamana baada ya matokeo ya uchaguzi Uturuki

Waandamana baada ya matokeo ya uchaguzi Uturuki

Jeshi la polisi nchini Uturuki limekandamiza maandamano ya Wakurdi waliomiminika barabarani kupinga matokeo ya uchaguzi nchini humo. Shirika la habari la Ufaransa limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, maandamano hayo yamefanyika kusini mwa Uturuki. Maandamano hayo yamefanyika baada ya kutangazwa matokeo ya awali ya uchaguzi wa bunge nchini Uturuki yanaonyesha kuwa chama tawala cha cha Uadilifu na Maendeleo (AKP) kinaongoza. Habari zinasema kuwa, 99% ya kura zilizohesabiwa hadi sasa inaonyesha kuwa chama hicho kimejizolea 49.3% ya kura hizo, kikifuatwa na chama cha Republican CHP kilichopata 25.2%. Chama cha Nationalist Movement MHP kimepata 12% ya kura hizo huku chama cha Kikurdi cha HDP kikijinyakulia 10.4% ya kura hizo. Vituo vya kupiga kura vilifungwa mwendo wa saa 11 jioni saa za nchi hiyo. Waturuki milioni 54 walikuwa wametimiza masharti ya kupiga kura kuchagua wabunge 550 ingawa haijabainika iwapo walishiriki zoezi hilo la kidemokrasia. Uchaguzi huo unaotazamiwa kumaliza kipindi cha miezi kadhaa ya hali ya wasiwasi na ya kukosekana kwa usalama nchini Uturuki unafuatiliwa kwa karibu na wengi wanangojea kuona kama chama cha AKP kilichoasisiwa na Rais Recep Tayyip Erdogan kitaweza kujipatia kura nyingi za kukiwezesha kuongoza serikali peke yake au la.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …