Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 27 Oktoba 2015 20:14

China yaifurusha meli ya Marekani katika maji yake

China yaifurusha meli ya Marekani katika maji yake

Wizara ya Ulinzi ya China imetangaza kuwa, meli zake za kivita zimeifurusha meli ya kivita ya Marekani baada ya meli hiyo kuingia katika maji karibu na kisiwa kinachogombaniwa cha bahari ya Uchina.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, awali Idara ya Usalama ya China ilifuatilia nyendo za meli hiyo ya Marekani aina ya 'USS Lassen' kabla ya kuionya kukaribia kisiwa hicho kwenye pwani ya China. Taarifa hiyo imesema China inaitaka Marekani irekebishe mienendo yake na iombe radhi haraka. Vilevile imeitaka Washington kuacha kufuata mkondo hatari au wa kichokozi dhidi ya taifa na maslahi ya China. Wizara ya Ulinzi ya China pia imesema kuwa, imekwishawasilisha malalamiko yake kwa Washington kutokana na meli zake za kivita kutishia usalama wa nchi hilo. Imeongeza kuwa, kitendo cha meli hizo za Marekani kupita eneo hilo na licha ya kutolewa mara kadhaa maonyo kutoka serikali ya Beijing, kunadhihirisha kiburi cha Marekani cha kutoheshimu haki ya kujitawala ya nchi nyingine. China pia imemwita balozi wa Marekani nchini humo katika Wizara ya Mambo ya Nje na kuwasilisha malalamiko ya Beijing kwa serikali ya Washington.
Weledi wa mambo wameitaja hatua ya Marekani ya kutuma meli yake ya kivita katika maji ya Uchina kuwa ya makusudi hasa kwa kuzingatia kuwa, kabla ya hapo viongozi wa Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo, Pentagon walitangaza azma yao ya kutuma meli za kivita katika visiwa vya Nansha au Spratly kama vinavyoitwa na wapinzani wa Beijing, vinavyodhibitiwa na Uchina, na kwamba katika safari hiyo, meli hizo zingesindikizwa na ndege za upelelezi. China ilianza kudhibiti visiwa hivyo mwaka jana 2014 baada ya kushadidi mzozo baina yake na nchi za Japan, Ufilipino, Malaysia, Taiwan, Brunei na Vietnam. Visiwa vya Spratly vinaaminiwa kuwa na utajiri wa mafuta na gesi mbali na umuhimu wake wa kistratijia.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …