Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 26 Oktoba 2015 19:48

Mamia wafariki dunia katika zilzala Afghanistan

Mamia wafariki dunia katika zilzala Afghanistan

Mtetemeko mkubwa wa ardhi uliokuwa na nguvu ya 7.5 kwa kipimo cha Rishta umetokea leo katika majira ya karibu saa nane mchana katika nchi kadhaa za Asia zikiwemo Afghanistan, Pakistan, India na Tajikistan. Zilzala hiyo pia imesikika huko China, Uzbekistan na Kyrgyzstan na hadi kufikia sasa mamia ya watu wamefariki dunia na kujeruhiwa kufuatia zilzala hiyo.

Shirika la Habari la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mashirika mengine ya habari za nje yameripoti kuwa, mtetemeko huo wa ardhi ambao kitovu chake kilikuwa ni kaskazini mashariki mwa Afghanistan, hadi sasa umeuwa na kujeruhi mamia ya watu, huku idadi ya watu walioaga dunia ikiongezeka. Habari kutoka katika mikoa mbalimbali ya Afghanistan zinasema kuwa, makumi ya nyumba zimebomoka na raia wamepata hasara na maafa mbalimbali.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …