Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 16 Oktoba 2015 11:46

Obama akiuka ahadi ya kuondoa majeshi Afghanistan

Obama akiuka ahadi ya kuondoa majeshi Afghanistan

Rais Barack Obama wa Marekani, amekiuka ahadi yake ya kuondoa majeshi ya nchi yake huko Afghanistan kufikia mwishoni mwa mwaka ujao na badala yake ametangaza kwamba wanajeshi hao wataendela kuwepo huko hadi hali ya mambo itakapoimarika.
Rais wa Marekani amedai kwamba hatua yake hiyo inatokana na eti kushindwa jeshi la Afghanistan kusimamia kikamilifu usalama wa nchi yao. Rais Obama anatumia mashambulizi ya kundi la Taliban dhidi ya mji wa Kunduz hivi majuzi kutetea hatua yake hiyo. Takriban wanajeshi 10,000 wa Marekani wataendelea kuwepo nchini Afghanistan hadi mwishoni mwa mwaka ujao na baadaye idadi hiyo itapunguzwa hadi 5,500. Wanajeshi watakaobaki Afghanistan wataendelea kuwa huko kwa muda usiojulikana. Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Ash Carter ametangaza kwamba, ameanza mazungumzo na nchi waitifaki ili kuziomba nazo zibakishe majeshi nchini Afghanistan hata baada ya 2017.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …