Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 04 Februari 2015 15:39

Makumi ya magaidi waangamizwa nchini Syria

Makumi ya magaidi waangamizwa nchini Syria

Jeshi la Syria limeendelea na operesheni zake dhidi ya makundi ya kigaidi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na kuwaangamiza makumi ya magaidi. Ripoti kutoka Syria zinasema kuwa, jeshi la nchi hiyo limewaangamiza magaidi 18 ambao ni wanachama wa makundi ya kigaidi ya Ahrar Sham na Jabhat al-Nusra katika eneo la al-Zabadan huko Rif Dimashq. Wakati huo huo Abu Muslim a-Tunis kiongozi wa Jabhat al-Nusra katika kijiji cha Sinai ameuawa pamoja na wanachama wengine kadhaa wa kundi hilo la kigaidi kufuatia operesheni ya kijeshi ya jeshi la Syria katika maeneo hayo. Aidha magaidi kadhaa wameuawa magharibi mwa medani ya al-Balidah baada ya kushambuliwa na wanajeshi wa nchi hiyo. Hayo yanajiri katika hali ambayo, habari kutoka nchini Syria zinabainisha kwamba, operesheni za jeshi la nchi hiyo dhidi ya makundi ya kigaidi zinaendelea kupata mafanikio kila siku.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …