Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 28 Disemba 2014 19:37

Vikosi vya kigeni vyamaliza operesheni Afghanistan

Vikosi vya kigeni vyamaliza operesheni  Afghanistan

Vikosi vya kigeni vinavyoongozwa na Marekani vimemaliza rasmi operesheni yao leo Jumapili kwa kuondoa idadi kubwa ya askari wake katika maeneo tofauti ya nchi hiyo iliyoharibiwa vibaya na vita. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa sherehe maalumu zilitarajiwa kufanyika leo mjini Kabul, kuadhimisha kumalizwa rasmi operesheni za kijeshi za vikosi vya kigeni nchini Afghanistan. Wanajeshi wasiopungua 13,500 wa kigeni wengi wao wakiwa ni kutoka na Marekani watabakia nchini Afghanistan kuisaidia serikali ya nchi hiyo kupambana na ugaidi. Hivi karibuni Marekani na Afghanistan zilitia saini makubaliano yaliyodaiwa ya pande mbili ambapo kwa mujibu wa makubaliano hayo, wanajeshi wa Marekani watabakia nchini Afghanistan hadi baada ya mwaka huu wa 2014 wakati wa kumalizika operesheni zao nchini humo. Askari wa NATO wanasema kuwa wataendelea kubakia nchini Afghanistan kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa askari wa nchi hiyo katika kupambana na ugaidi. Mwaka 2001 Marekani iliongoza mashambulizi yaliyoipindua serikali ya Taliban nchini Afghanistan, hata hivyo nchi hiyo imeendelea kukosa usalama hadi leo hii. Kwa mujibu wa mtandao wa icasualitie.org, wanajeshi wa kigeni 3500 wameuawa nchini Afghanistan tangu mwaka 2001 wakati Marekani ilipoivamia nchi hiyo kwa madai ya kupambana na ugaidi.

 

 

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …