Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 14 Aprili 2016 12:25

B/Haram waonyesha video ya wasichana wa Chibok

Kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram nchini Nigeria, limeonyesha mkanda wa video unaowaonyesha wasichana 15 wanaosadikiwa kutekwa nyara mwaka 2014 katika shule ya sekondari ya Chibok nchi humo.
Ndege za kijeshi nchini Nigeria zimeshambulia ngome muhimu ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram na kulitia hasara kubwa.
Alkhamisi, 14 Aprili 2016 11:52

Watu 46 wameuawa nchini Burundi mwaka huu

Watu 46 wameripotiwa kuuawa ndani ya kipindi cha miezi mitatu ya mwanzoni mwa mwaka huu katika ghasia zinazoendelea nchini Burundi.
Alkhamisi, 14 Aprili 2016 09:22

Kipindupindu chaua watu kadhaa Zambia

Watu kadhaa wamepoteza maisha kutokana na kusambaa ugonjwa wa kipindupindu katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Nigeria imesisitiza juu ya ulazima wa kuzidishwa mawasiliano na ushirikiano unaohitajika kati ya nchi za eneo ili kupambana na kundi la Boko Haram.
Alkhamisi, 14 Aprili 2016 08:18

Watu watatu wauawa katika mripuko Somalia

Watu watatu wameuawa na wengine wasiopungua sita kujeruhiwa katika mlipuko ulitokea jana Jumatano katika soko lililokuwa na watu wengi huko Somalia.
Serikali ya Ivory Coast imewataka raia wa nchi hiyo ambao wamekimbilia katika nchi jirani na kuomba hifadhi ya ukimbizi kurejea nchini kwao.
Waziri Mkuu mpya wa Madagascar amekabidhiwa ofisi leo na kuanza rasmi kuhudumu katika wadhifa huo huku akiahidi kupambana na umasikini na ufisadi.
Rais Peter Mutharika wa Malawi ametangaza hali ya maafa nchini humo kufuatia ukame mkubwa uliosababisha kupungua pakubwa mavuno ya kilimo.
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, inasikitishwa na hatima isiyojulikana ya wanafunzi wa kike waliotekwa nyara na kundi la kigaidi la Boko Haram mnamo mwaka 2104.
Mahakama ya Juu ya utawala wa kizayuni wa Israel imepitisha kuwa, nyaraka za mauzo ya silaha ya utawala huo haramu kwa serikali ya Rwanda wakati wa mauaji ya kimbari katika …
Makamu kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini amewasili katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba, katika fremu ya makubaliano ya amani.
Mripuko wa homa ya manjano umesababisha vifo vya watu wasiopungua 21 katika Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo.
Watu kadhaa wameuawa na kujeruhiwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya waasi wa Uganda kufanya mashambulizi kwenye maeneo hayo.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tunisia imesema kuwa imelikamata kundi moja la kigaidi katika mkoa wa Bizerte kaskazini mwa nchi hiyo.
Karibu miili 350 ya Waislamu imepatikana ikiwa imezikwa kwa siri katika kaburi la umati kaskazini mwa Nigeria.
Kundi la magaidi wakufurishaji wa Boko Haram nchini Nigeria wanazidi kuwatumia watoto wadogo kusheheni bomu na kujiripua katika hujuma za kigaidi.
Jumanne, 12 Aprili 2016 20:38

Watu watano wauawa sokoni nchini Burundi

Watu watano wamepigwa risasi na kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa Jumatatu usiku kufuatia hujuma iliyofanyika katika soko moja mashariki mwa Burundi.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya amesema kuwa uingiliaji kijeshi wa nchi za Magharibi nchini humo ulikuwa makosa.
Askari wa waasi nchini Sudan Kusini wamerejea mjini Juba, mji mkuu wa nchi hiyo katika kuanza kutekelezwa makubaliano ya amani kati ya serikali na upinzani nchini humo.

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …