Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 30 Aprili 2016 08:42

Algeria yawaachilia wachimba migodi wa Chad

Algeria yawaachilia wachimba migodi wa Chad
Wizara ya Mambo ya Mahakama nchini Chad imetangaza kuachiliwa huru wachimba mgodi 103 raia wa nchi hiyo ambao walikuwa wakishikiliwa nchini Algeria kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, wachimba migodi hao tayari wameshawasili N'Djamena, mji mkuu wa Chad. Imesema kuwa, watu hao wameachiliwa baada ya Waziri wa Masuala ya Mahakama ya Chad kulifuatilia suala hilo huko Algeria. Kwa mujibu wa afisa mmoja wa Wizara hiyo ya Vyombo vya Mahakama na ambaye hakutaka kutaja jina lake, wachimbamigodi hao wanaojishughulisha na uchimbaji dhahabu katika milima ya Tibesti inayoishia kaskazini mwa nchi hiyo, walitiwa mbaroni na askari wa Algeria mwaka mmoja uliopita na kuzuiliwa nchini humo kwa kipindi chote hicho. Baadhi ya duru zimesema kuwa, wachimba migodi hao wameachiliwa huru kufuatia msamaha wa Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria ambaye ameamua kuwasamehe raia hao wa Chad. Wachimbaji hao wadogowadogo wa madini kutoka Chad hupendelea sana kufanya shughuli zao katika milima ya Tibesti, na wakati mwingine wanavuka mmpaka na kuingia Niger na kufika hadi katika ardhi ya Algeria kupitia Nigeri kwa ajili ya kuchimba dhahabu kinyume cha sheria.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …