Katika tukio la kwanza Ijumaa mchana watu wanne wamefariki baada ya ukuta kuporomoka na kuwaangukia mtaani Kilimani kati ya ubalozi wa Russia na makao makuu ya idara ya ulinzi DOD.
Aidha watu watatu wamethibitishwa kupoteza maisha katika mtaa wa Huruma jijini Nairobi baada ya jingo la ghorifa sita kuporomoka Ijumaa usiku kufuatia mvua kali. Maafisa wa uokoaji wangali wanaendelea kuwatafuta watu wanaoaminika kuwa chini ya vifusi vya jengo hilo ambalo inasemkana likuwa na familia 150 ndani yake.
Baadhi ya barabara jijini Nairobi zilifurika na kutatiza usafiri kutokana na mvua inayozidi kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini. Barabara iliyoathirika zaidi ni barabara kuu ya Thika maeneo ya Parklands. Mtaa wa South C pia uliathirika huku wakazi wa Komarock pia wakiathirika kwa maji yaliyoingia ndani ya nyumba zao. Mitaro ya kuelekezxa maji nje ya barabara inasemekana kujaa taka ambayo ilisababisha barabara hizo kufurika, hata hivyo baadhi ya wenyeji wamelalamika kuwa hakuna mipango madhubuti ya kuelekeza maji kwengineko.