Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 29 Aprili 2016 20:42

Waislamu wa Nigeria wataka uwazi jinai za Zaria

Waislamu wa Nigeria wataka uwazi jinai za Zaria

Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria imeendelea kusisitizia umuhimu wa kuwekwa wazi mauaji ya wanajeshi wa nchi hiyo dhidi ya Waislamu katika mji wa Zaria mwishoni mwa mwaka jana 2015.

Harakati hiyo ya Kiislamu kwa mara nyingine tena imelituhumu jeshi la Nigeria kwa kuwaua kwa umati Waislamu katika mji wa Zaria na kutaka kufukuliwa miili yote ya wahanga wa jinai hizo waliozikwa katika kaburi moja la umati ili ukweli ujulikane. Hii ni katika hali ambayo siku ya Jumanne Waislamu wa Nigeria walifanya maandamano makubwa ya kwenda kwenye kaburi hilo la umati huko Mando, pambizoni mwa mjini Kaduna wa kaskazini mwa Nigeria. Itakumbukwa kuwa tarehe 14 Disemba mwaka jana, siku moja baada ya jeshi la Nigeria kufanya mauaji ya kinyama dhidi ya Waislamu katika mji wa Zaria, liliizika miili ya wahanga hao katika kaburi moja kwa lengo la kuficha ushahidi wa ukubwa wa jinai hiyo. Mbali na harakati hiyo kutaka miili ya wahanga hao ifukuliwe, imelaani hatua ya serikali ya Rais Muhammadu Buhari ya kupotosha ukweli kwa kudai kuwa katika kaburi hilo ilizikwa miili ya watu 347 pekee katika hali ambayo karibu watu 1000 waliuliwa na jeshi la nchi hiyo. Hayo yanajiri ikiwa ni siku chache baada ya Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International kutangaza kuwa, jeshi la Nigeria liliua zaidi ya Waislamu 350 wanachama wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria inayoongozwa na Sheikh Ibrahim Zakzaky mwezi Disemba mwaka jana.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …