Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 29 Aprili 2016 20:41

Hatma ya Zuma kitendawili, mahakama yamsakama

Hatma ya Zuma kitendawili, mahakama yamsakama

Mahakama kuu ya Afrika Kusini imetolea hukumu kuhusu tuhuma za huko nyuma zinazomkabili Rais Jacob Zuma wa nchi hiyo.

Sambamba na kutoa hukumu hiyo, mahakama kuu ya mjini Pretoria imesema kuwa, uamuzi uliotolewa mwaka 2009 wa kutupilia mbali tuhuma za ufisadi wa kiuchumi dhidi ya Rais Zuma, haukuwa na mantiki. Hii ni katika hali ambayo wapinzani wa serikali na timu ya wanasheria nchini humo wanaamini kwamba, uamuzi wa mwaka 2009 wa kufuta mashtaka dhidi ya rais huyo si tu haukuwa na mantiki, lakini pia ulitolewa kwa msingi wa kisiasa. Kwa mujibu wa mahakama Kuu ya Afrika Kusini, uchunguzi wa faili hilo bado unaendelea kwa ajili ya kuweka wazi hali za pande zote mbili katika kesi hiyo. Tuhuma hizo zinahusiana na manunuzi ya silaha yenye gharama za mabilioni ya dola hapo mwaka 1999 ambapo kwa mujibu wake, kipindi hicho Afrika Kusini ilitumia mabilioni ya dola kununua silaha za kivita kutoka shirika moja la silaha la nchini Ufaransa.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …