Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 28 Aprili 2016 12:10

Askari wa UN CAR waongezewa muda wa kuhudumu

Askari wa UN CAR waongezewa muda wa kuhudumu

Askari wa kofia ya buluu wa Umoja wa Mataifa wanaosimamia amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, wameongezewa muda wa kuhudu nchini humo.

Hatua hiyo imechukuliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa baada ya kupasisha azimio nambari 2281, ambapo kwa mujibu wa azimio hilo askari hao watatakiwa kusalia nchini humo hadi tarehe 31 mwezi Julai mwaka huu. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, sanjari na kuongezwa muhula wa miezi mitatu kwa askari hao wa UN, vikosi hivyo vinaweza kutumia mfumo wa kistratijia kuandaa mazingira kwa ajili ya kuhitimisha shughuli zao nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia wameitaka serikali mpya ya Rais Faustin-Archange Touadéra kutangaza shughuli mpya za askari hao ambazo pia zinaendana na mazingira ya sasa. Kwa kipindi cha miaka miwili tangu askari hao wa Umoja wa Mataifa wawasili nchini humo, wamesaidia kusimamia uchaguzi mkuu sanjari na kuanzisha operesheni za kukusanya silaha kutoka kwa makundi ya wabeba silaha. Mgogoro wa ndani nchini Jamhuri ya Afrika ya kati, uliibuka katikati ya mwaka 2013. Katika kujaribu kuhitimisha mauaji nchini humo, UN iliamua kutuma karibu askari elfu 12 hapo mwaka 2014 chini ya mwamvuli wa vikosi vya kusimamia amani nchini humo, MINUSCA.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …