Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 28 Aprili 2016 12:05

Raia 16 wa Misri wauawa kwa kupigwa risasi Libya

Raia 16 wa Misri wauawa kwa kupigwa risasi Libya

Duru za habari nchini Libya zimeripoti kuuawa raia 16 wa Misri kufuatia ufyatulianaji risasi na wafanya biashara ya magendo katika eneo la Bani Walid kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa habari hiyo raia hao wa Misri waliokuwa wanakusudia kuhajiri kinyume cha sheria kuelekea Libya na kisha Ulaya, wameuawa baada ya kupigwa risasi na wafanyabiashara ya magendo katika eneo hilo. Wakati huo huo, Ahmed Abu Zeid, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri ameutaka ubalozi wa nchi yake huko Libya kufanya mawasiliano na viongozi wa eneo la Bani Walid na pia serikali ya umoja wa kitaifa nchini Libya ili kufahamu kiini cha kujiri tukio hilo. Abu Zeid pia ameutaka ubalozi huo kuchukua hatua za haraka ili kufahamu utambulisho wa wahanga wa mauaji hayo na kuirejesha miili yao nchini kwao. Hii ni katika hali ambayo mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Mataifa nchini Libya, Martin Kobler amelaani mauaji dhidi ya raia hao wa Misri na kutaka kufanyike uchunguzi wa haraka kubaini wahusika, kama ambavyo pia ametaka kurejeshwa utawala wa kisheria katika eneo la Bani Walid. Itafahamika kuwa raia wengi wa Misri wapo nchini Libya wakishughulisha na kazi mbalimbali. Wengi wa Wamisri hao wanafanya kazi za ujenzi nchini humo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …