Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 28 Aprili 2016 11:59

USA: Tunapanga kuiwekea vikwazo Sudan Kusini

USA: Tunapanga kuiwekea vikwazo Sudan Kusini

Serikali ya Marekani imewaonya viongozi wa Sudan Kusini kuwa, watakabiliwa na vikwazo ikiwa hawatoheshimu makubaliano ya amani.

Donald Booth, mwakilishi wa Marekani nchini Sudan na Sudan Kusini ameyasema hayo akihutubia kongresi ya nchi yake na kuongeza kuwa, Washington iko katika kuchunguza namna ya kuiadhibu serikali ya Juba kukiwemo kuiwekea vikwazo vya silaha. Amesema kuwa hatua hizo zitachukuliwa endapo Sudan Kusini itashindwa kutoa ushirikiano mzuri kwa ajili ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa ili kuhitimisha mgogoro wa ndani nchini humo. Aidha Booth ameongeza kuwa, Washington imeweka machaguo yote mezani na kwamba iko tayari kuchunguza uwezekano wa kuiadhibu nchi hiyo changa zaidi barani Afrika katika sekta ya silaha. Katika sehemu nyingine Marekani imekutaja kurejea mjini Juba Riek Machar, kinara wa upinzani kuwa ni hatua muhimu katika kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa. Machar aliapishwa kuwa makamu wa rais siku ya Jumanne. Hatua ya Rais Salva Kiir ya kumtimua Machar kutoka nafasi ya umakamu wa rais, iliingiza Sudan Kusini katika vita vya ndani hapo mwezi Disemba mwaka 2013 ambapo maelfu ya raia wameuawa na mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi. Vita nchini Sudan vilikaribia kulisambaratisha kabisa taifa hilo lililoamua kujitenga na Sudan mwaka 2011.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …