Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 28 Aprili 2016 08:26

Umoja wa Mataifa waitaka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kulitafutia ufumbuzi tatizo la wakimbizi

Umoja wa Mataifa waitaka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kulitafutia ufumbuzi tatizo la wakimbizi
Umoja wa Mataifa umeitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutafuta ufumbuzi wa kudumu kuhusiana na wakimbizi wa mashariki mwa nchi hiyo.

Taarifa ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa, serikali ya Kinshasa inapaswa kuandaa mipango ya kudumu kwa ajili ya wakimbizi wanaoyakimbia makazi yao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Chaloka Beyani, ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya haki za binadamu kwa wakimbizi amesema baada ya kufanya safari ya siku sita katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwamba, kutokana na maeneo kadhaa ya Kivu Kaskazini kufungwa, kuna wakimbizi wengi ambao wako msituni.

Hii ni katika hali ambayo, siku chache zilizopita Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) ilionesha wasiwasi wake kuhusiana na hali ya zaidi ya raia elfu 35 waliokimbia mapigano katika eneo la Mpati huko Kivu Kaskazini.

Aidha inaelezwa kuwa, hali ya kibinadamu katika maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inazidi kuwa mbaya siku baada ya siku.

Hali mbaya na machafuko katika maeneo hayo ni kikwazo kikuu cha kuwafikishia misaada ya kibinadamu wahitaji.

Kwa miaka kadhaa sasa maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamekuwa yakishuhudia machafuko na ghasia zinazosababishwa na mgogoro wa makundi ya waasi yanayoendesha shughuli zao katika maeneo hayo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …