Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatano, 27 Aprili 2016 18:53

Wanaoshiriki vita dhidi ya B/Haram watekeleze ahadi

Wanaoshiriki vita dhidi ya B/Haram watekeleze ahadi

Mkuu wa vikosi vya Kiafrika vya kupambana na kundi la kigaidi la Boko Haram amezitaka nchi zinazoshiriki katika operesheni ya kijeshi dhidi ya wanamgambo hao kufungamana na ahadi zao.

Lamidi Adeosun, kamanda wa operesheni ya kupambana na Boko Haram ambaye ni raia wa Nigeria ameonesha kusikitishwa kwake na hatua ya nchi zinazoshiriki katika operesheni hiyo kutotekeleza ahadi zao. Kamanda Lamidi amesema kuwa, washiriki wote wa operesheni hiyo walipaswa kutekeleza ahadi zao kama walivyokuwa wameahidi.

Mkuu wa kikosi cha Kiafrika cha kupambana na kundi la Boko Haram amesema hayo akiwa nchini Niger ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mahamadou Issoufou wa nchi hiyo pamoja na mkuu wa majeshi ya nchi hiyo.

Kamanda Lamidi amesema kuwa, kwa sasa kundi la Boko Haram halidhibiti mji au kijiji chochote kile na kwamba, wanachama wake wamelazimika kwenda kujificha katika maeneo ya mbali kando kando ya Ziwa Chad.

Ripoti zinaonesha kuwa, kundi la Boko Haram lililoanzisha machafuko ya ndani nchini Nigeria mwaka 2009 limeua zaidi ya watu elfu 20 na kulazimisha mamilioni ya wengine kukimbia maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo. Kundi hilo pia limepanua wigo wa mashambulizi yake ya kigaidi katika nchi jirani kama Cameroon, Chad na Niger na kuhatarisha usalama wa raia.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …