Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 26 Aprili 2016 19:01

Machar, Mkuu wa waasi Sudan Kusini aapishwa kuwa makamu wa rais

Machar, Mkuu wa waasi Sudan Kusini aapishwa kuwa makamu wa rais

Kiongozi wa waasi Sudan Kusini Riek Machar amewasili katika mji mkuu wa nchi hiyo, Juba na kuapishwa kuwa makamu wa rais wa nchi hiyo.

Machar ameapishwa kuwa makamu wa rais katika serikali inayoongozwa na hasimu wake wa muda mrefu, Rais Salva Kiir. Machar alichelewesha kuwasili Juba kwa miezi kadhaa jambo ambalo liliikasirisha jumuiya ya kimataifa ambayo imehusika katika kuwaleta mahasimu hao wawili pamoja ili wagawane madaraka katika nchi hiyo changa zaidi duniani.

Vita vya ndani nchini humo vilivyoanza Disemba 2013 vimesababisha mauaji ya maelfu ya watu na kulazimisha mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi. Nchi hiyo ilitumbukia katika vita vya ndani baada ya Rais Salva Kiir kutoka kabila la Dinka kumtuhumu makamu wake za zamani, Riek Machar wa kabila la Nuer kwamba alihusika na jaribio la kupindua serikali yake.

Kwa mujibu wa mapatano ya amani yaliyotiwa saini Addis Ababa Ethiopia, kutakuwa na serikali ya mpito itakayodumu kwa muda wa miezi 30. Kiir atachukua asilimia 53 ya viti serikalini huku upande wa Machar ukipata asilimia 33 na wafungwa wa zamani wa kisiasa na vyama vingine vya kisiasa vikipata asilimia 7 kila mmoja.

 

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …