Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 25 Aprili 2016 21:04

CORD wapigwa mabomu ya kutoa machozi Kenya

CORD wapigwa mabomu ya kutoa machozi Kenya

Viongozi wa Muungano wa CORD wa Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga na wafuasi wao wamekumbwa na zahama kubwa leo baada ya polisi kuwafyatulia mabomu ya kutoa machozi katika jaribio la kutawanya maandamano yao mbele ya jengo la Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC jijini Nairobi.

Muungano wa CORD umeitisha maandamano hayo ili kushinikiza maafisa wa tume hiyo ya uchaguzi wajiuzulu.

Makumi ya maafisa wa polisi walimiminwa kwenye jengo la Anniversary Towers ambamo ndimo zilimo ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya. Maafisa hao wa polisi walipewa amri moja tu ya kutoruhusu kufanyika maandamano yoyote kwenye eneo hilo. Polisi imewataka waliopanga maandamano hayo wavunje mpango huo na badala yake watafute njia nyingine za kutatua matatizo yao. Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Nairobi, Japheth Koome alikuwa amesema mepama kuwa, wafuasi wa CORD hawataruhusiwa kuingia kwenye ofisi za IEBC. Polisi waliendelea kusimama imara leo mbele ya jengo hilo wakati wafuasi wa CORD walipokuwa wanapiga firimbi na kusema "mapambano bado" nje ya jengo hilo kabla ya askari hao kuwafyatulia mabomu ya kutoa machozi wafuasi hao wa CORD na viongozi wao. Katika upande mwingine shughuli za tume ya IEBC ziliendelea kama kawaida, bila ya kuathiriwa na maandamano hayo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …