Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 25 Aprili 2016 19:36

WHO: Malaria itaangamizwa Afrika hadi mwaka 2020

WHO: Malaria itaangamizwa Afrika hadi mwaka 2020

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, kuna uwezekano ugonjwa wa malaria utaangamizwa kabisa ifikapo mwaka 2020.

Ripoti iliyotolewa leo na WHO kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Malaria imesema kuwa, kuna uwezekano kwamba ugonjwa huo utakomeshwa kabisa katika nchi sita za Afrika zinazosumbuliwa sana na malaria hadi kufikia mwaka 2020. Ripoti hiyo imeongeza kuwa, nchi hizo ni Algeria, Cape Varde, Swaziland, Bostwana, Afrika Kusini na Comoro.

Afrika Kusini imetangaza suala la kupambana na malaria kuwa ni lengo la kitaifa.

Takwimu zinaonesha kuwa, eneo la chini ya Sahara barani Afrika ndilo lenye idadi kubwa zaidi ya kesi za ugonjwa wa malaria unaosababishwa na mbu aina ya Anopheles. Asilia 88 ya wagonjwa wa malaria na asilimia 90 ya vifo vilivyosababishwa na ugonjwa huo katika mwaka uliopita wa 2015 iliripotiwa katika eneo hilo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …