Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 25 Aprili 2016 19:36

Faili la hali ya Burundi lafunguliwa mahakama ya ICC

Faili la hali ya Burundi lafunguliwa mahakama ya ICC

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC imefungua faili maalumu la kufuatilia hali ya kisiasa na kiusalama ya Burundi.

Bi Fatou Bensouda, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC amenukuliwa na shirika la habari la Ufaransa akisema leo kuwa, kumefunguliwa faili maalumu la kufuatilia hali ya Burundi ambayo tangu mwaka jana imekumbwa na machafuko ya kisiasa.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa mahakama ya ICC amesema, wamekuwa wakifuatilia kwa karibu matukio ya Burundi tangu mwezi Aprili 2015 na mara kadhaa wamekuwa wakizitaka pande hasimu nchini huyo zijiweke mbali na machafuko.

Fatou Bensouda ameongeza kuwa, mahakama ya ICC imewaonya kwa mara kadhaa baadhi ya watu nchini Burundi kuhusu uwezekano wa kutendeka jinai nchini humo na namna mahakama hiyo inavyofuatilia kwa karibu kila linalojiri huko Burundi.

Burundi ilitumbukia katika machafuko tangu mwezi Aprili 2015 baada ya wapinzani kupinga hatua ya chama tawala cha CNDD-FDD ya kumuidhinisha Rais Pierre Nkurunzinza kugombea tena urais kwa kipindi cha tatu mfululizo.

Taarifa zinasema kuwa, zaidi ya watu 400 wameshauwa na zaidi ya laki mbili na 50 elfu wamelazimika kuwa wakimbizi nje ya Burundi kutokana na machafuko hayo.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …