Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 25 Aprili 2016 11:33

Jeshi la Nigeria lawaua wapiganaji 10 wa Boko Haram

Jeshi la Nigeria lawaua wapiganaji 10 wa Boko Haram

Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa, limewauwa wanachama wasiopungua 10 wa kundi la kigaidi la Boko Haram mashariki mwa jimbo la Borno lililoko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Sani Usman, msemaji wa jeshi la Nigeria ametangaza kuwa, wanachama hao wa Boko Haram wameuawa katika operesheni ya jeshi katika jimbo la Birno na kwamba, kuna raia kadhaa waliokuwa wakishikiliwa mateka na wanamgambo hao ambao wamekombolewa na jeshi.

Msemaji wa jeshi la Nigeria ameongeza kuwa, lengo la operesheni hiyo ni kuyasafisha kabisa maeneo ya jimbo la Borno na uwepo wa wanamgambo hao wa Boko Haram ambao wamekuwa wakifanya mauaji ya kiholela dhidi ya raia.

Kundi la Boko Haram lililoanzisha machafuko ya ndani nchini Nigeria mwaka 2009 limeua zaidi ya watu elfu 20 na kulazimisha mamilioni ya wengine kukimbia maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo. Kundi hilo pia limepanua mashambulizi yake ya kigaidi katika nchi jirani kama Cameroon, Chad na Niger.

Serikali ya Nigeria imeendelea kukosolewa kutokana na kushindwa kulitokomeza kabisa kundi hilo la Boko Haram ambalo sasa limepanua wigo wa harakati zake mpaka katika maeneo ya nchi jirani.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …