Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 25 Aprili 2016 11:30

Watu 14 wauawa katika mapigano ya kikabila Ethiopia

Watu 14 wauawa katika mapigano ya kikabila Ethiopia

Watu wasiopungua 14 wameuawa nchini Ethiopia na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya kuzuka mapiganao makali ya kikabila katika eneo moja nchini humo.

Vyombo vya usalama vya Ethiopia vinaripoti kwamba, mapigano hayo yaliyotokea magharibi mwa Ethiopia yaliibuka baada ya gari moja la shirika la misaada lililokuwa likiendeshwa na dereva Muethiopia kuwagonga na kuwauawa watoto wawili wa kabila la Nuer katika kambi ya wakimbizi wa Sudan Kusini.

Baada ya tukio hilo kundi la wakimbizi wa Sudan Kusini liliwavamia na kuwauwa wanaume na wanawake Waethiopia walioko jirani na maeneo ya kando kando na kambi hiyo ya wakimbizi.

Katika mapigano hayo raia 10 Waethiopia wameuawa na wakimbizi wanne wa Sudan Kusini. Baada ya kuibuka mapigano hayo, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wale wa Shirika la Madakrati Wasio na Mipaka walilazimika kuondoka katika maeneo hayo wakihofia usalama wa maisha yao na kwenda katika hoteli za mji wa Gambela.

Baadhi ya raia wa Ethiopia walio na hasira wameshambulia ofisi za Umoja wa Mataifa na za mashirika ya misaada ya kibinadamu wakisema kuwa, mashirika hayo yanawasaidia wakimbizi ambao wanawaua Waethiopia walioko katika nchi yao.

Ikumbukwe kuwa, tarehe 15 mwezi huu watu wenye silaha wasiojulikana kutoka Sudan Kusini walishambulia eneo la Gambela lililoko magharibi mwa Ethiopia, na kuua watu 208 na kujeruhi wengine 75. Eneo la Gambela na mkoa wa jirani na eneo hilo yamewapa hifadhi wakimbizi zaidi ya laki mbili kutoka Sudan Kusini waliokimbia mapigano nchini kwao.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …